MAN UNITED YATOLEWA CARABAO CUP LICHA YA ZLATAN IBRAHIMOVIC KUFUNGA

PAKUA APPS KALI INAYOKUPA VITU VIZURI VYOTE BONYEZA HAPA 
Mambo yanaendelea kuwa mabaya kwa Manchester United, hiyo ni baada ya kutolewa katika Kombe la Carabao kwa kufungwa mabao 2-1 na Bristol City.
Man United ambayo ilipanga kikosi tofauti kidogo na kile kinachotomika kwenye Premier League ilipata bao lake pakee kupitia kwa straika mkongwe Zlatan Ibrahimovic aliyefunga katika dakika ya 58 baada ya Bristol City kutangulia kufunga kupitia kwa Joe Bryan katika dakika ya 51.
Bao la pili lilifungwa na Korey Smith katika dakika ya 92 baada ya timu yake kufanya kazi nzuri ya kuwatoka walinzi wa Man United.
Mchezo huo ulikuwa ni wa robo fainali ya Carabao Cup ambapo sasa Manchester City imepangwa kucheza dhidi ya Bristol City huku Chelsea ikicheza dhidi ya Arsenal katika hatua ya nusu fainali ambapo mechi za kwanza zitachezwa Januari mwakani.